Na Dixon Busagaga
SERIKALI imeahidi kuongeza kasi katika zoezi la ukamataji wa wahusika wa matukio ya mauaji yaliyotokea Kibiti,Rufiji na Mkuranga mkoani Pwani na kuhakiksha wanafikishwa mbele ya vyombo vya sharia.
SERIKALI imeahidi kuongeza kasi katika zoezi la ukamataji wa wahusika wa matukio ya mauaji yaliyotokea Kibiti,Rufiji na Mkuranga mkoani Pwani na kuhakiksha wanafikishwa mbele ya vyombo vya sharia.
Waziri
Mkuu wa Tanzania ,Kassim Majaliwa aliyasema hayo jana katika baraza la
Idd lililofanyika kitaifa katika mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro
lkitanguliwa na Swala ya Idd El Fitri iliyofanyika kitaifa katika
msikiti wa Riadha.
“Kinachofanyika
sasa nikuhakikisha kwanza tunawapata waharifu halisi ilikuepuka
kuingiza watu wasio husika, kama vile hao wenye hisia kwamba mauaji haya
yanafanywa labda na waislamu hapana .”alisema Mh Majaliwa .
Alisema
kaz kubwa inayofanywa sasa ni kuchuja na kujua nani hasa anashiriki
katika mauaji hayo huku akiwashukuru watanzania ambao tayari wameanza
kutoa ushirikiano kwa kuanza kueleza nani wanahusika katika tukio hilo.
“Kazi
yetu ni kuwapeleleza pale ambapo tunauthibitisho wa ushiriki wao na
hatua kali zitachukuliwa dhidi yao na kazi hiyo inaendelea vizuri.”alisema Majaliwa.
Mapema
katika taarifa ya Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) iliyosomwa
na kaimu katibu Mkuu,Sheakh Salim Amir Abeid alisema Bakwata imeshtushwa
na matukio ya mauaji ya kutisha ya watu wasio na hatia katika maeneo ya
mkoa wa Pwani.
Alisema
kutokana na matukio hayo Baraza kuu linatoa pole kwa familia
zilizopoteza ndugu na jamaa zao katika matukio hayo aliyoyataja kutokuwa
na hata chembe ya kibinadamu .
“Kumekuwepo
na matukio ya kutisha ya mauaji ya watu wasio na hatia katika maeneo ya
mkoa wa Pwani,matukio ambayo yametushtua sana na kuisikitisha mioyo
yetu,baraza kuu la waislamu la Tanzania kwanza kabisa linatoa pole kwa
familia zilizopoteza ndugu na jamaa zao katika matukio hayo ya kinyama
yasio na chembe ya kibinadamu hata kidogo.”alisema Abeid
Alisema
Bakwata inasikitishwa na vitendo vyenye viashiria vya kutaka kuichafua
dhima nzuri ya Tanzania kuwa ni kisiwa cha amani na utulivu hasa pale
matukio hayo yanapo husishwa na na Dini ya Kiislamu.
“Uislamu
ni dini ya amani upendo kuvumilia na nakuishi pamoja na watu wa imani
tofauti na kwamba yeyote afanyae matendo yoyote na kinyama kama hayo
katu haiwakilishi uislamu na baraza linawataka waislamu kushikamana.”alisema Abeid.
0 comments:
Chapisha Maoni