Mahakama ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi imemhukumu kwenda jela miaka 23 mkazi wa kijiji cha Kalovye, Osward Mpalasinge (26).
Amepewa
adhabu hiyo baada ya kupatikana na hatia ya kuvunja na kuiba vitu
mbalimbali ikiwemo cheti cha kidato cha nne. Hukumu hiyo ilitolewa jana
na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Teotimus Swai baada ya mshtakiwa
kukiri kosa mahakamani.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Swai alisema mtuhumiwa amekutwa na hatia pasipo shaka hivyo anahukumiwa kwenda jela miaka 23.
Awali,
Mwendesha Mashitaka, Baraka Hongoli alisema mshitakiwa alitenda makosa
ya kuvunja na kuiba Mei 25 mwaka huu saa mbili usiku nyumbani kwa
Veronica Crispin katika Kijiji cha Kalovye, Inyonga.
Alidai
kwamba mshitakiwa alifika nyumbani hapo, akavunja na kisha kuiba nguo
zenye thamani ya Sh 110,000 na cheti cha kidato cha nne cha Henreth
Edward Kalamu, kilichotolewa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA)
mwaka 2015.
Hongoli
aliitaka mahakama kutoa adhabu kali kwa mtu huyo ili iwe fundisho kwa
kuwa wizi wa aina hiyo ndio umesababisha usumbufu na watu kupoteza ajira
zao serikalini na maeneo mengine pindi uhakiki wa vyeti unapofanyika.
Akijitetea, mshitakiwa aliiomba mahakama impatie muda ili aweze kwenda Dar es Salaam kumtafutia mtu huyo cheti kingine
0 comments:
Chapisha Maoni