test

Jumatatu, 12 Juni 2017

EWURA Wasitisha Mchakato wa Kuiongezea Leseni Kampuni ya IPTL......Ni Baada ya Waziri Mkuu kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu


Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesitisha mchakato wa kushughulikia maombi ya IPTL ya kuongezewa muda wa leseni yake ya biashara kwa miezi 55 ili iendelee kuzalisha umeme na kuiuzia TANESCO.

Mbali na kusitisha mchakato huo, EWURA imesitisha pia upokeaji wa maoni kutoka kwa umma na wadau mbalimbali kuhusu kusudio lake la kuiongezea muda wa kufanyakazi nchini Kampuni ya IPTL

Uamuzi huu wa EWURA umekuja ikiwa ni siku moja baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi bila kueleza sababu za uamuzi huo.

Hapa chini ni taarifa ya EWURA

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni