Mbunge
wa Mkuranga kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdallah Ulega
amewafananisha wabunge wa upinzani na popo kuwa hawaeleweki na kusema
wamekuwa watetezi wa wawekezaji ambao wao wamewatuhumu kuwa ni wezi wa
madini.
Mbunge
huyo amesema hayo bungeni akisema kuwa wapinzani hao leo limewashuka
baada ya jana Rais Magufuli kukutana na Mwenyekiti wa Kampuni ya
Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia
Mining Limited Prof. John L. Thornton na kukubaliana kuwa kampuni hiyo
ipo tayari kufanya mazungumzo na Serikali ya Tanzania ili kulipa fedha
ambazo Tanzania imezipoteza kutokana na kampuni hiyo kuendesha shughuli
zake hapa nchini.
"Popo
hajafahamika kama ni mnyama au ndege mpaka hivi leo na hawa wenzetu
hata sitaki kuwaita vinyonga naomba niwaite popo maanake hawajafahamika
kama ndege au wanyama na leo limewashuka kwani walijigeuza kuwa mawakili
wa wale ambao sisi tunawatuhumu kwamba ni wezi wetu na yule anayehusika
Mkuu amewathibitishia mchana wa leo (jana) ameingia na amekiri mwenyewe
kwa kinywa chake ya kwamba wapo tayari kulipa pesa ambazo tunawadai na
tena lile lililokuwa linaonekana jambo gumu la kujenga kinu cha
kuchenjua madini amelichukua na amesema yupo tayari kujenga" alisema Ulega
Mbunge
huyo alikwenda mbali zaidi na kesema bara la Afrika limekuwa na bahati
mbaya kwani wapinzani wa Afrika wamekuwa wakitumika na mabeberu miaka
yote na kusema wao kama Chama Cha Mapinduzi wanakila sababu ya kutamba
kwa kuwa Ilani ya Uchaguzi ya CCM imeweka sawa na kutamka namna nzuri ya
kusimamia shughuli za madini.
==>Msikilize hapo chini
==>Msikilize hapo chini
0 comments:
Chapisha Maoni