Mamilioni ya watanzania
watapata fursa ya kuishuhudia timu yetu ya vijana - Serengeti boys
inayoshiriki michuano ya vijana ya AFCON Mbashara kupitia king’amuzi
cha DStv.
Michuano hiyo itakayoanza 14 hadi 28 mwezi
huu wa Mei itashirikisha mataifa 8 kutoka bara la Africa.
Michuano hiyo itaonekana
mubashara kupitia king’amuzi cha DStv tena katika kifurushi cha bei
nafuu kabisa cha Bomba, kinachopatikana kwa shilingi 19,975/= na hivyo
kuwawezesha watanzania wengi zaidi kuwashuhudia
vijana wetu wanavyopambana kuliletea taifa sifa katika ulingo wa
kandanda.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Multichoice Tanzania Maharage Chande, amesema kuwa kitendo cha michuano
hiyo kuonekana kwenye vifurushi vyote vya DStv, kinamaanisha watanzania
tutashuhudia mtanange huo Mubashara tena kwa
kiwango cha juu, hivyo kuupata uhundo huo ukiwa bado wa moto.
“Tunafahamu ni jinsi gani watanzania wanasubiri kwa hamu kuwaona vijana
wetu wanavyopambana kufa na kupona, hivyo sisi DStv, tumeamua kuonyesha
michuano hiyo live tena katika vifurushi vyote hadi
kile cha bei nafuu kabisa cha Bomba ambacho ni shilingi 29975 tu.”
Alisema Maharage.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi
huyo, michuano hiyo itaonekana katika chaneli 209-SuperSport9 na
chaneli 233-SuperSport Select, ambayo pia inapatikana katika kifurushi
cha Bomba.
Huku michuano hii
ikiaminika kuwa moja ya nafasi muafaka kwa Serengeti boys kufuzu kwenda
Kombe la Dunia la vijana litakalofanyika nchini india mwishoni mwa mwaka
huu, Watanzania wengi wanaimani na timu hiyo hasa
ukizingatia mazoezi waliyofanya ikiwemo michezo ya majaribio pamoja na
muda waliokaa kambini.
Serengeti Boys watacheza
mechi yao ya kwanza siku ya Jumatatu 15 Mei kabla ya kukabiliana na
Angola siku ta Alhamisi 18 Mei na hatimaye Niger siku ya Jumapili 21
Mei.
Matumaini makubwa ya
watanzania yapo kwenye kikosi hicho imara chenye wachezaji mahiri kama
Nickson Kababage, Shaaban Ada na Kelvin Nashon ambao wanatarajiwa
kuongoza mashambulizi makali ya kuwabomoa mahasimu
wao katika michuani hii.
Michuano
ya AFCON kwa wachezaji wenye umri wa miaka chini ya 17 ya mwaka huu ni
ya 12 kwa kuzingatia michuano inayohusisha nchi waandaaji, inayoandaliwa
na shirikisho la soka barani Afrika (CAF) kwa wachezaji wenye umri wa
chini ya miaka 17.
Washindi wane watapata tiketi ya kushiriki michuano
ya Kombe la Dunia la wachezaji wa umri wa chini ya miaka 17
litakalofanyika ncini India mwishoni mwa mwaka huu.
Michuano ya mwaka huu
ilipaswa ifanyike nchini Madagascar tarehe 2–16 April 2017 lakini CAF
ikaamua kuihamishia Gabon kwa sababu Madagascar haikukidhi vigezo.
Mataifa yaliyofuzu kushiriki michuano hii mwaka huu ni wenyeji Gabon, Tanzania, Mali,
Angola, Cameroon, Ghana, Guinea, na Niger.www.dstv.com.