Siku chache
baada ya DStv kutangaza kuwa itarusha moja kwa moja (Mubashara)
Michuano ya vijana ya AFCON itakayoanza kesho huko Gabon, habari mpya na
njema zinasema sasa DStv itarusha mechi zote za
Serengeti boys katika michuano hiyo kwa lugha ya Kiswahili.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande, amesema baada ya
kampuni yake kuhakikisha kuwa michuano hiyo inashuhudiwa mubashara
kupitia DStv, sasa wanataka watanzania wengi zaidi
waweze kuifuatilia kwa karibu hususan mechi za timu yetu ya Serengeti
Boys, hivyo mechi zote za Serengeti boys zitarushwa mubashara kwa lugha
ya Kiswahili.
Amesema
watangazaji na wachambuzi mahiri wa mpira wakiwemo Abuubakar Lyongo,
Maulid Kitenge, Ephraem Kibonde, Edo Kumwembe na Maestor watashiriki
katika zoezi hilo la kuwaletea watanzania burudani
hiyo kupitia DStv.
“DStv
tunatoa huduma wanayotaka wateja wetu, tunawasikiliza wateja wetu, na
kila inapowezekana tunatekeleza matakwa yao” alisema Maharage na
kuongeza kuwa baada ya watu kufahamu kuwa DStv itarusha
michuano hiyo mubashara, kumekuwa na maombi mengi ya kuangalia
uwezekano wa kutangaza michuano hiyo hususan mechi za Serengeti boys kwa
Kiswahili.
“Tunaamini
kuwa kwa kurusha matangazo hayo kwa Kiswahili, watanzania wa kila kada
wataweza kuifuatilia michuano hiyo kwa ukaribu zaidi na hivyo kuongeza
burudani ya aina yake katika michuano hiyo”
alisema Maharage na kuongeza kuwa pamoja na kutangaza kwa Kiswahili,
pia wamehakikisha michuano hiyo inaonekana katika vifurushi vyote
kikiwemo cha Bomba cha Sh. 19,975tu ambacho ni miongoni mwa vifurushi
nafuu kabisa hapa nchini.
Amewataka
watanzania wote kuendelea kuiunga mkono timu yetu kwa kila hali kwani ni
muwakilishi wa taifa letu katika michuano hiyo muhimu. “Sisi DStv ni
wazalendo wa kweli, ndiyo sababu hatusiti kuunga
mkono timu zetu wakati huohuo tukiwahakikishia watanzania fursa ya
kushuhudia mashindano mbalimbali mubashara. Enzi za kuangalia micezo
iliyonakiliwa imepita, na sisi watanzania tunaenda sambamba na ulimwengu
wa kisasa. Kupitia DStv, tunaona vitu mubashara”
alisema Maharage.
Serengeti
Boys watacheza mechi yao ya kwanza siku ya Jumatatu 15 Mei kabla ya
kukabiliana na Angola siku ya Alhamisi 18 Mei na hatimaye Niger siku ya
Jumapili 21 Mei.
Kwa mujibu
wa majadiliano mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii, watanzania wengi
wanasubiri kwa shauku michuano hiyo huku ikionekana wazi kuwa wanaimani
na Serengeti boys.
Michuano
ya AFCON kwa wachezaji wenye umri wa miaka chini ya 17 ya mwaka huu ni
ya 12 kwa kuzingatia michuano inayohusisha nchi waandaaji,
inayoandaliwa na shirikisho la soka barani Afrika (CAF) kwa wachezaji
wenye umri wa chini ya miaka 17. Washindi wane watapata tiketi ya
kushiriki michuano ya Kombe la Dunia la wachezaji wa umri wa chini ya
miaka 17 litakalofanyika ncini India mwishoni mwa
mwaka huu.
Michuano ya
mwaka huu ilipaswa ifanyike nchini Madagascar tarehe 2–16 April 2017
lakini CAF ikaamua kuihamishia Gabon kwa sababu Madagascar haikukidhi
vigezo.
Mataifa yaliyofuzu kushiriki michuano hii mwaka huu ni wenyeji Gabon, Tanzania, Mali,
Angola, Cameroon, Ghana, Guinea, na Niger.