Waziri
wa mambo ya ndani ya nchi Mhe.Mwigulu Nchemba amewaonya wananchi wa
Kibiti mkoa wa Pwani kutowaficha wahalifu wanaofanya mauaji mkoani humo
bali wawafichue ila maisha yaweze kuendelea kama zamani na kudai pasipo
kufanya hivyo kuna gharama.
Mhe.
Mwigulu amewataka wananchi kutambua kwamba kuendelea kuwaficha wahalifu
waliopo ndani ya jamii watambue kuna gharama kubwa ambayo itawafanya
maisha yasiweze kusonga mbele.
Mwigulu
ameyasema hayo jana Kata ya Bungu wilaya ya Kibiti mkoa wa Pwani mara
baada yakutembelea majeruhi na kambi maalum ya jeshi la Polisi mkoani
humo kwa ajili ya kupambana na waalifu ambao wanajihusisha na kuua
wananchi ,viongozi wa dini na vyama.
Wakati
akizungumza na wananchi pamoja na kikosi maalumu kilichopo huko, Mhe.
Mwigulu amesema kwamba serikali imejipanga vyema kubana mianya ya wote
wanaofanya mauaji hayo na kuongeza kwamba itawatia nguvuni, na kuwataka
wananchi kuwa mstari wa mbele kuwafichua wahalifu hao
Nchemba
ameendelea kufunguka kwamba uhalifu unaoendelea kwa sasa maeneo hayo
ya Kibiti yanasababisha wasiwasi kwa wananchi na kuongeza kuwa serikali
haitawaacha wahalifu waendelee kufanya mauaji hayo na kuongeza kwamba
hakuna ruhusa ya aina yeyote ya mtu kumuua mwenzake kwa misingi yakua na
mtazamo tofauti wa dini, chama , kabila na asili.
Pamoja
na hayo ameongeza kwamba serikali imeanza kuwabaini wahusika wa vitendo
hivyo na bado wanaendelea na uchunguzi ili kuwabaini wahalifu wengine.
==>Msikilize hapo chini akiongea
==>Msikilize hapo chini akiongea
0 comments:
Chapisha Maoni