Askofu
wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema Serikali
inapaswa kuwashirikisha viongozi wa dini katika kupambana na mauaji ya
Polisi na raia yanayoendelea kutokea katika wilaya za Kibiti, Mkuranga
na Rufiji mkoani Pwani.
Akihubiri
katika Ibada ya Jumapili jana kwenye kanisa lake lililoko Ubungo jijini
Dar es Salaam, Askofu Gwajima alisema mauaji hayo ni roho kamili ambayo
pamoja na sheria za nchi, inapaswa kuondolewa kwa maombi.
Alifafanua
kuwa Jeshi la Polisi nchini na dola wanazuia uhalifu kimwili, lakini
viongozi wa dini wanazuia ki roho, hivyo wote wanatakiwa kushirikiana
ili kukomesha matukio hayo ya mauaji yanayoleta hofu kwa watu.
"Kiongozi
wa dini anaweza kwenda Kibiti na kuwaambia walioua polisi na kuendeleza
mauaji wajitokeze na kusalimisha silaha na wakaja, lakini watu hao
wakiitwa na Polisi walete silaha hawatatokea,' alisema.
Akitumia
mfano wa mahubiri aliyosema kuwa aliwahi kuyatoa mwaka 1995 eneo la
Kibiakali, Gwajima alisema viongozi wa dini wana nguvu ya ziada
kupambana na uhalifu.
"Mimi
nimewahi kuhubiri mwaka 1995 huko Kibiakali na kusema kuwa waliokuwa
wanamiliki silaha walete kwa jina la Yesu na nilifanikiwa kukusanya SMG
nane ambazo walileta kwa mikono yao," alieleza.
"Hivyo,
tunaomba (viongozi wa dini) Serikali itupatie nafasi ya kuhubiri ili
kuweza kupambana na roho hizo za mauaji. Pia huu ni wakati wa Kanisa
kulia na kusali ili kuweza kupambana na vita hivi vya kiroho ambayo
inahitaji nguvu ya rohoni kukamata wahalifu.
Katika hatua nyingine Askofu Gwajima alisema Tanzania ni nchi iliyobarikiwa, hivyo siyo vyema watu wakaitabiria mabaya.
Ameyasema
hayo jana wakati wa Ibada ya Jumapili kanisani kwake Ubungo. Alisema
kuna jambo ambalo Mungu atafanya ambalo litaonyesha dhahiri kuwa
Tanzania ni nchi tajiri.
"Watanzania
ni makuhani wa nchi, tumezaliwa nchi hii tumekunywa maji katika nchi
hii, hivyo hatupo radhi kuona watu wanatabiri vitu ambavyo havipo
katika utabiri."
Aliendelea "Wiki
iliyopia nilisema baadhi ya watu ambao walikuwa wanafanya Tanzania
shamba la bibi kwa kila mtu kuilani nchi hii, wanatakiwa kujua kuwa
Tanzania ni nchi iliyobarikiwa.
Pia
itafika wakati mataifa yatajua kuwa nchi hii ni tajiri hivyo viongozi
wa dini na waumini wanatakiwa kuiombea ili mpango wa Mungu uweze
kutimia.
"Na
ndio maana hivi karibuni nimekuwa mkali kwa baadhi ya manabii
wanaotabiri mabaya katika Taifa hili sipo radhi kuona watu wanatabiri
mambo ambayo hayaendani na nchi hii kwani hivi karibuni Mungu
atajidhirisha katika nchi hii ambayo ipo kwa makusudi yake"alisema.
Aliongeza
kuwa wapo watu ambao wataona aibu nchi hii siku ambayo Mungu
atajidhihirisha na kuiweka juu, hata hivyo waumini na viongozi
wanatakiwa kuitabiria mema nchi na kuiombea ili baraka zake zishuke.
"Mungu
alimwambia Sauli toka uende, na utakapokuwa unakwenda utakutana na
manabii watakao kuwa wanatabiri roho ya Bwana atashuka na kuwa mtu
mwingine, Leo hii waumini mbalimbali wametoka sehemu tofauti na kuja
kusikia utabiri huu. Sisi ni mabalozi wa Mungu hapa duniani.
Alifafanua
kuwa Kanisa halitakiwa kulilia demokrasia bali linatakiwa kulilia
Ufalme kwamba ule ushawishi wa mbinguni Mungu akisema ndio hakuna wa
kupinga, bali mtafuata tu hata kama wengi wanasema lakini watafuata tu.
Baadaye sheria ijae Katiba ya Mungu, Sheria ya Mungu na tusimame katika mlima Kilimanjaro na kutangaza neema na ufalme wa Mungu.
Gwajima
alisema wanasiasa hawaaminiki na kuwataka Watanzania kuweka tumaini lao
kwa Mungu ambaye ndiye anayeweza kuwapa msaada wa kweli.
"Unafikiri
wanasiasa wanaweza kuibadili nchi? Je, una mtazamo huo? Ukimtembelea
mwanasiasa mmoja na mwingine ni kama leo unamtembelea chui na kesho
simba. Usiweke tumaini juu yao, weka tumaini lako kwa Mungu"
0 comments:
Chapisha Maoni