Timu
ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imetolewa
katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17, baada ya kufungwa
1-0 na Niger katika mchezo wa mwisho wa Kundi B Uwanja wa Port Gentil
mjini Gentil, Gabon.
Matokeo
hayo yanazifanya Niger na Tanzania kuwa sawa kwa pointi na wastani wa
mabao ya kufunga na kufungwa, hivyo mshindi katika mechi baina yao
amefuzu Kombe la Dunia Oktoba mwaka huu India na pia kwenda Nusu Fainali
ya michuano hiyo.
Kwa
matokeo hayo Niger inaungana na Mali ambayo inaongoza kundi kwa pointi
zake saba, baada ya ushindi wa mechi mbili na sare moja, wakati Tanzania
na Angola zote zikiaga mashindano hayo.
Kwa
ujumla, Serengeti Boys ilizidiwa katika mchezo huo kwa kipindi cha
kwanza na cha pili hali iliendelea kuwa hivyo na hatimaye Niger wakatoka
kifua mbele kwa kuitoa Tanzania.
0 comments:
Chapisha Maoni