test

Jumatatu, 15 Mei 2017

TOTTENHAM WAUWAGA UWANJA WA WHITE HART LANE KWA USHINDI DHIDI YA MAN UNITED


KLABU ya Tottenham Hotspurs kutoka London siku ya jana katika mchezo dhidi ya Manchester United walifanikiwa kufanya tafrija ya kuuwaga uwanja wao wa White Hart Lane ambao waliutumia katika kipindi chao chote.


Tottenham imefanya sherehe hizi kutokana na kwamba hawataweza kuutumia uwanja huu tena kwa kupisha ukarabati wa uwanja huu wa White Hart Lane ambao unahitajika kutanuliwa tofauti na ulivyo sasa.
Katika sherehe hizi waliweza kuhudhuria watu mashuhuri hasa wachezaji wakubwa ambao walipita katika klabu hiyo kama Dimitor Berbatov alikuwepo.

Hivyo basi Tottenham itaanza kuutumia rasmi uwanja wa taifa wa Wembley katika msimu ujao wa kiufanya ndio uwanja wao wa nyumbani,kwaajili ya kupisha ujenzi ambao umeanza rasmi katika uwanja huo.

Katika mchezo wa round 36 ambao walicheza na klabu ya Manchester United hapo jana,Spurs walifanikiwa kushinda ushindi wa mabao 2-1.
Magoli yalifungwa na Victor Wanyama na Harry Kane huku la Man United likifungwa na Wayne Rooney.

MATOKEO YA MECHI ZA JANA PREMIER LEAGUE

▪England - Premier League


☆FT Crystal Palace 4 - 0 Hull City

☆FT West Ham United 0 - 4 Liverpool

☆FT Tottenham Hotspur 2 - 1 Manchester United.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni