Mtazamo wa haraka haraka bila kuumiza akili ni kwamba,Hans Poppe anaondoka kwenye kamati ya usajili klabuni hapo.
Inadaiwa kwamba Mwenyekiti huyu wa kamati hii ya usajili ndugu yetu Hans Poppe hakuridhishwa na namna viongozi wa juu wa klabu ya Simba walivyoshiriki katika mchakato wa mkataba mpya na kampuni ya ubashiri ya SportPesa yenye maskani yao makuu nchini Kenya.
“Waliamua kufanya mambo kwa uficho na hadi wanasaini mkataba hakukuwa na uwazi wa mambo. Sitaki kuwa sehemu ya maamuzi ambayo yanakiuka uungwana."
Klabu ya Simba imeingia mkataba wa Sh bilioni 4.9 pesa za kitanzania ambao utadumu kwa miaka mitano.
0 comments:
Chapisha Maoni