Shambulizi
la kihalifu mitandaoni lililotendeka kupitia vifaa vinavyoaminika
kuibwa kutoka kitengo cha ujasusi nchini Marekani NSA limeathiri
mashirika tofauti duniani.
Kampuni
ya kulinda uhalifu wa mitandao Avast, imesema kuwa imeona kesi 75,000
za programu zinazotumika kufanya uhalifu mtandaoni inayojulikana kama 'WannaCry' duniani.
Kuna ripoti za maambukizi katika mataifa 99 ikiwemo Urusi.
Kati ya mashirika yalioathirika zaidi ni shirika la huduma za afya nchini Uingereza na Uskochi.
Programu
hiyo ilisambaa kwa kasi siku ya Ijumaa ambapo ilitaka malipo ya dola
300 ili kufungua faili ilizokuwa imeziteka nyara katika kompyuta.Siku
nzima, mataifa ya Ulaya yaliripoti maambukizi hayo.
==> Hii ni Tahadhari Iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA kuhusu Kirusi hicho