Hatimaye
siku iliyokuwa imesubiriwa kwa hamu na Watanzania ya kuishuhudia timu
yao ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imefika
ambapo, leo Jumatatu inafungua pazia lake katika mashindano ya Kombe la
Afrika kwa Vijana, kwa kumenyana na Mali katika michuano hiyo
inayofanyika nchini Gabon.
Aidha,
Serengeti Boys imepangwa katika Kundi B, ambapo katika kundi hilo iko
pamoja na timu nyingine za Angola na Niger ambazo nazo zitakuwa
kibaruani leo.
Kocha
Mkuu wa timu hiyo, Bakari Shime amesema kuwa kikosi cha Serengeti Boys
kiko vizuri na kimejiandaa vya kutosha kuwakabili vijana wa mali kwenye
mchezo huo wa kwanza.
“Kikosi
kipo vizuri na tumejipanga kuikabili vilivyo timu ya Mali kwani
tunataka kuwafurahisha Watanzania kwa kutowaangusha na naomba wazidi
kutuombea,” amesema Bakari Shime.
Timu hiyo ya Taifa ya vijana pamoja na maandalizi mazuri lakini imepata pigo baada ya nahodha, Abd Makamba kuvunjika mguu hivyo hataweza kushiriki mashindano yote.
"Ni
jambo la kusikitisha kidogo kwamba Nahodha wetu Issa Abdi Makamba
alipata mpasuko wa mguu juzi mazoezini kwa bahati mbaya akiwa pekee yake
kabisa…Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa madaktari wangu wamesema kwamba
hatoweza kushiriki mashindano haya na jina lake tumeliondoa katika
mashindano tayari nafasi yake imeshachukuliwa na mtu mwingine kwa sababu
tulikuwa na wachezaji wa akiba". Alisema Shime na kuongeza;
“Imekuwa
bahati mbaya kwetu, bahati mbaya kwa Issa Abdi amepambana kwa miaka
miwili kuiongoza hii timu kuhakikisha inafikia hapa ambapo imefika
lakini tunaamini mchango wake ni mkubwa sana na kwa sababu bado yupo
ndani ya kikosi anaendelea na majukumu yake kama Kapteni kuhamasisha na
kuongoza wenzake bado tunampa pole Issa Abdi tunaamini kabisa wachezaji
wanatakiwa kupigana kwaajili yake”.
0 comments:
Chapisha Maoni