Jackline
Ngalo ambaye ni Mwanasheria wa shirika la kutetea Haki za watoto
wafanyakazi wa nyumbani nchini, WOTESAWA, akizungumza na Lake Fm, baada
ya semina kwa viongozi wa serikali za Kata/Mitaa pamoja na wadau wengine
wa maendeleo katika wilaya za Ilemela na Nyamagana mkoani Mwanza ili
kuwajengea uwezo wa kutetea haki za watoto wafanyakazi wa nyumbani
katika maeneo yao.
Semina
kwa viongozi wa serikali za Mitaa pamoja na wadau wengine wa maendeleo
katika wilaya za Ilemela na Nyamagana mkoani Mwanza ikiendelea Jijini
Mwanza
Semina hiyo imeandaliwa na shirika la WOTESAWA kwa siku tatu tangu Mei 09 hadi leo Mei 11,2017
Washiriki wa semina hiyo wakimsikiliza mwanahabari Nashon Kenedy, wakati akichangia mada kwenye semina hiyo
Wadau
wa Maendeleo mkoani Mwanza wameidhinisha mikakati mbalimbali ikiwemo
kufanya sensa ya watoto wafanyakazi wa nyumbani na utungwaji wa sheria
ndogo ndogo za kuwalinda watoto, lengo likiwa ni kusaidia mapambano
dhidi ya ukatili kwa watoto hao.
Wamefikia
makubaliano hayo leo kwenye kilele cha mafunzo ya siku tatu kwa
viongozi wa serikali za mitaa kutoka Wilaya za Nyamagana na Ilemela
yaliyoandaliwa na Shirika la kutetea Haki za watoto wafanyakazi wa
nyumbani la WOTESAWA lililopo Jijini Mwanza.
Akizungumzia
mikakati hiyo, Jackline Ngalo ambaye ni Mwanasheria wa shirika la
WOTESAWA amebainisha kwamba, mikakati hiyo itasaidia kuwalinda watoto
wafanyakazi wa nyumbani ikiwemo kuwanusuru na utumikishwaji wa kazi
nzito huku wakilipwa ujira mdogo.
Wadau
walioafiki mikakati hiyo ni Madiwani, Watendaji wa Kata, Wenyeviti wa
Mitaa, Maafisa Ustawi na Maendeleo ya Jamii ambapo wameongeza kwamba
mafunzo hayo yatawasaidia kuielimisha jamii kupitia mikutano ya hadhara
ili kuepukana na ukatili kwa watoto hususani wafanyakazi wa nyumbani.
Baadhi
ya watoto wamekuwa wakikosa fursa ya kusoma kutokana na kuajiriwa
katika kazi za nyumbani kinyume na sheria huku wakilipwa ujira mdogo
tofauti na waraka wamishahara wa mwaka 2013 unavyoelekeza.