Mbunge
wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa
amesikitishwa sana na matokeo ya uchaguzi wa Bunge la Afrika Mashariki
(EALA) uliofanyika jana usiku bungeni mjini Dodoma kwa upande wa
Chadema.
Kupitia
ukurasa wake wa Facebook Zitto ameandika kuwa kuchagua watu bila
kuangalia uwezo, uzoefu na uhusika wao kulingana na sehemu wanapotakiwa
kuwepo ni kuliangamiza taifa, hasa ukizingatia changamoto zilizopo
katika nchi hizo Afrika Masahriki.
Amesema
kuwa nchi kama Rwanda, Burundi na Uganda zimepeleka wawakilishi
mashuhuri na wenye uzoefu mkubwa katika bunge hilo kulingana na umuhimu
wa shughuli zinazofanywa na bunge hilo.
“Jana
usiku nilikuwa na hasira sana, kufuatia matokeo ya uchaguzi wa
wawakilishi wa Tanzania kwenye bunge la Afrika Mashariki (EALA)
haiwezekani kuchagua wabunge ambao hawana uwezo wa kwenda kujenga hoja,
huku tukitegemea kupambana na changamoto za muungano wa nchi hizi za
Afrika Mashariki”ameandika Zitto katika ukurasa wake wa Facebook.