Viongozi wa
muungano wa Nasa, Kalonzo Musyoka (kushoto) Moses Wetang'ula, Isaac
Ruto, Musalia Mudavadi na Raila Odinga Aprili 27, 2017 wakiwa Uhuru
Park. Picha/DENNIS ONSONGO
Kwenye mkakati huo, NASA pia imetangaza kununua kamera na zaidi ya simu 40,000 maalum ili kuewawezesha kurekodi kila matukio yanayojiri katika vituo hivyo, hasa wakati kuhesabu kura kwenye Uchaguzi Mkuu wa Agosti.
Kwenye mkakati huo, NASA pia imetangaza kununua kamera na zaidi ya simu 40,000 maalum ili kuewawezesha kurekodi kila matukio yanayojiri katika vituo hivyo, hasa wakati kuhesabu kura kwenye Uchaguzi Mkuu wa Agosti.
Wakiwahutubia wakazi wa Kaunti ya Isiolo mnamo Jumatano wakati wa
mkutano wa kisiasa, kiongozi wa muungano huo Raila Odinga alisema kwamba
hawataacha nafasi yoyote kwa “wizi wa kura kuendeshwa na serikali ya
Jubilee”.
Bw Odinga, aliye pia mgombea urais, alisema watakuwa wakinakili na
kutengeneza sajili yao mpya kila baada ya saa tatu, ili kuhakikisha
kwamba hakuna “wageni” wanaoshiriki katika upigaji kura.
“Hakuna wageni watakaopiga kura mara hii, kinyume na walioorodheshwa
katika Sajili Kuu ya Kitaifa,” akasema Bw Odinga. Mgombea mwenza Kalonzo
Musyoka alisema kuwa wameziba mianya yoyote ambayo Jubilee inaweza
kutumia kuiba kura.
“Tumejipanga vilivyo. Mara hii hali ni tofauti sana. Tunataka kuwaambia
wenzetu Jubilee kwamba ikiwa walidhani wamerauka, sisi tushakesha na
kujipanga. Hawatakuwa na nafasi yoyote ya kuwahadaa Wakenya tena,”
akasema Bw Musyoka.
Aidha, Musyoka, alisema kwa simu hizo, maajenti hao watapiga picha
matokeo yatakayotangazwa katika vituo hivyo, ili kuyaweka kama ushahidi
ikiwa, Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) itajaribu kuyabadilisha katika
Kituo cha Kitaifa cha Kuhesabu Kura.
Wawili hao walikuwa wameandamana na vinara wenza Musalia Mudavadi (ANC),
Seneta Moses Wetang’ula (Bungoma) na mwenyekiti mpya wa Baraza la
Magavana (COG) Josephat Nanok, mbunge Junnet Mohammed (Suna Mashariki)
kati ya wengine.
Bw Wetang’ula alimwambia Naibu Rais William Ruto kukoma kuwatukana
viongozi wa NASA, huku akiifananisha Jubilee na chama cha KANU mnamo
2002 pamoja na kulinganisha NASA na uliokuwa muungano wa NARC.
Mudavadi alisema kuwa lengo lao ni kuibuka washindi kwa kishindo.
“Tunataka kuushinda uchaguzi huu katika duru ya kwanza. Tunawaomba wafuasi wetu kuamka mapema na kupiga kura zao.
0 comments:
Chapisha Maoni