test

Jumatatu, 5 Juni 2017

Polisi Moshi yazuia jeneza la mwili wa Ndesamburo Kutembezwa Barabarani


Jeshi la Polisi mkoa wa Kipolisi wa Moshi limezuia  utaratibu wa kutoa heshima za mwisho kwa kuutembeza katika barabara za viunga vya manispaa hiyo, mwili  aliyekuwa  Mwenyekiti wa Chadema, Kilimanjaro, marehemu Philemon  Ndesamburo .

 Majibu ya barua yaliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Polisi Moshi, yamezuia mwili huo kupitishwa katika barabara za kati kati ya mji kwa kile walichoeleza kuwa leo Juni 5 na siku ya kazi na kuna shughuli za mbalimbali zinazoendelea.

Sababu ya pili iliyotolewa na ofisi hiyo ni kwamba wakiupitisha mwili huo barabarani watasababisha msongamano mkubwa ambao utakuwa chanzo cha usumbufu  kwa watumiaji wengi wa barabarani.

“Ofisi ya Mkuu wa polisi wa wilaya inatoa maelekezo kuwa mwili wa Ndesamburo ukitolewa KCMC, upitishwe barabara ya YMCA kupitia Lucy Lameck Road hadi uwanja wa michezo wa Majengo ambapo kumepangwa kufanyika kwa shughuli zote za kutoa heshima za mwisho.

 Jana mmoja wa wanakamati ya mazishi ya Ndesamburo, Anthony Komu alisema  kuwa  mwili wa Ndesamburo utachukuliwa KCMC saa 4 asubuhi na kupitishwa katika barabara kuu za mji wa Moshi ili kuwawezesha ambao hawatapata nafasi ya kufika Majengo, kuuaga mwili huo.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni