Mdau
mkubwa wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘MO’ ameiandikia klabu hiyo
barua (demand note) ya kuitaka kumlipa fedha zote za mishahara alizokuwa
akiwalipa wachezaji tangu mwaka jana kiasi cha shilingi bilioni 1.4
baada ya kubaini kuwa klabu hiyo imeingia mkataba na kampuni ya
SportPesa bila kumshirikisha.
Hayo
yamejiri siku moja baada ya Simba kutiliana saini mkataba wa udhamini
na kampuni ya SportPesa. Uongozi wa Simba ukiongozwa na Rais wa timu,
Evans Aveva, ulisaini mkataba huo wa miaka mitano na kampuni ya
SportPesa wenye thamani ya Sh. 4.9 bilioni.
MO
amewaandikia Simba ‘demand note’ kwa kuwa wamekiuka makubaliano yao
kwamba, atoe fedha kama makubaliaono ya kuingia kwenye mfumo wa hisa na
ikitokea kampuni inataka kuidhamini Simba inabidi wakae meza moja
viongozi na MO ili hiyo kampuni itambue mwelekeo wa Simba, lakini
viongozi wa klabu hiyo wakasaini kimyakimya.
Klabu
hiyo ya Simba imeanza mchakato wa marekebisho ya katiba yao ili
kuruhusu kipengele cha uwekezaji kwa mfumo wa hisa kama lilivyokua ombi
la MO kuwekeza katika klabu hiyo kwa asilimia 51 za hisa huku wanachama
wakibaki na hasilimia 49.