test

Jumamosi, 13 Mei 2017

SAID MWAMBUNGU KUZIKWA KIJIJI CHA MIEMBENI WILAYA YA MALINYI MOROGORO


Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Said Thabiti Mwambungu anatarajia kuzikwa kesho jumapili katika kijiji alichozaliwa cha Miembeni wilaya ya Malinyi mkoa wa Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa familia, mwili wa marehemu Said Mwambungu utaondoka Dar es Salaam majira ya saa 11 jioni ya leo na kuwasili mkoani Morogoro majira ya kati saa 3 na saa 4 usiku.

Katika msafara huo utafikia moja kwa moja nyumbani kwa marehemu maeneo ya Kolla Hill kata ya Bigwa na kupumzika kwa muda wa saa moja kisha kuendelea na safari ya kuelekea kijiji cha Miembeni wilayani Malinyi kwa ajili ya mazishi yake.

Akizungumza   mjini hapa, Mwenyekiti wa Morogoro Press Club, Nikson Mkilanya ameomba waandishi wa habari kujitokeza kwa uwingi kupokea msiba huo na kutoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi huo.

Mkilanya alieleza kuwa Inshallah yeye ni miongozi mwa watu wataonda kumsitiri marehemu Said Mwambungu kwani kiongozi huyo alikuwa kioo katika tasnia ya habari wakati akiwa mkuu wa wilaya ya Morogoro kabla ya kuwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma.

"Binafsi nitaenda kumsindikiza Mzee Mwambungu hadi nyumbani kwake na kumsitiri na hii ni kwa niaba yangu na pia nitakuwa nawakilisha kundi kubwa la wanahabari wa morogoro lakini pia nitaungana na vijana wenzangu wengi wa mji wa Morogoro katika hili."alieleza Mkilanya.

Mkilanya alieleza kuwa Mwambungu ameacha kumbukumbu nzuri kwa waandishi wa habari hivyo njia pekee ya kukumbuka mazuri yake ni waandishi kujitokeza katika kuupokea mwili wake na kutoa heshima za mwisho na alikuwa kiongozi wa mfano si kwa wanahabari tu bali hata kada nyingine.

Marehe Said Thabiti Mwambungu ameriki jana katika hospitali ya taifa ya Muhimbili akisumbuliwa na ugonjwa wa figo hadi umati ulimpokuta.

Tumuombee apumzike kwa amani katika maisha mapya ya kaburi sote tupo safari hiyo...inshallah.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx