Lwandamina aliyetokea Zesco ya Zambia kwa mara ya kwanza juzi Jumamosi alikiongoza kikosi hicho dhidi ya JKU kwenye mchezo wa kirafiki ambapo timu hiyo ilifungwa kwa mabao 2-0 Uwanja wa Uhuru, Dar.
Lwandamina amesema kwamba lengo kubwa la kuchukua maamuzi hayo ya kukibomoa kikosi hicho ni kutaka kuangalia uwezo wa mchezaji mmojammoja na yule ambaye ataonyesha uwezo ndiye ataingia kwenye timu yake.
“Sina kikosi cha kwanza mpaka sasa kwani bado naangalia wachezaji wote viwango vyao na yule ambaye ataonyesha uwezo ndiye ataingia kwenye timu yangu na utaona hilo nimeanza kulifanya kwenye mechi na JKU ambapo nimewatumia wachezaji wote.
“Lengo ni kumtazama kila mmoja na kujua anafiti wapi na yupi anastahili kuanza na nani awe mbadala wa mwenzake, lakini suala la matokeo lisiwape watu hofu kwani hatukuwa tunaangalia zaidi kupata matokeo ila kuangalia viwango vya wachezaji wangu.
“Niwapongeze wapinzani wetu kwani walipata nafasi na kutumia vizuri lakini sisi hatukufanikiwa kufanya hivyo hata hivyo huu ni mwanzo na nimeshajua wapi pana upungufu wa kuufanyia kazi,” alisema Lwandamina.
SHARE THIS
Share on FacebookTweet on TwitterPlus on Google+