Kwa mujibu wa baraza la mawaziri la nchi hiyo wamekubaliana kuwa uchaguzi huo utafanyika Agosti 4 ya mwakani huku Rais Paul Kagame akitarajiwa kugombea tena kwa muhula wa tatu baada ya kubadilishwa kwa katiba yanchi hiyo.
Naye Kasisi wa zamani wa kanisa la Katholiki, Joseph Nahimana anayeishi nchini Ufaransa kama mkimbizi alitangaza kutaka kugombea urais kupitia chama cha upinzani wiki chache zilizopita lakini hali imekuwa tofauti baada ya kuzuiwa kuingia nchini humo.
Mpaka sasa serikali ya Rwanda haijazungumzia lolote kuhusu sababu ya kuzuiwa kwa kasisi huyo kuingia nchini humo.