Video hizo zimeonekana kutoana nduki kwa mashabiki wao kuziangalia mara nyingi zaidi zikigusa rekodi ya kuangaliwa zaidi ya mara milioni moja ndani ya kipindi kisichozidi wiki mbili tangu zilipopandishwa mtandaoni.
Muziki ya Darassa imeshaangaliwa zaidi ya mara milioni 1.43 tangu ilipopandishwa kwenye mtandao huo Novemba 23 mwaka huu huku ‘Dume Suruali’ ikiangaliwa zaidi ya mara milioni 1.13 tangu ilipowekwa YouTube Novemba 25 mwaka huu.
Hii inaonesha kuwa hivi sasa wasanii wanaungwa mkono zaidi na mashabiki wao kwa kuangalia video zao kwenye mtandao kutokana na uwepo wa mapinduzi ya kiteknlojia, ambapo mamilioni ya Watanzania sasa wanaweza kupata ‘internet’ kwenye simu zao.