Mauzo
ya Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) yameshuka katika kipindi cha
wiki iliyopita kwa 91% kutoka Tsh 32.5 Bilioni na kufikia Tsh 3 Billion.
Pia Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa zimeshuka kwa 94% kutoka 9
millioni hadi laki 5.
Afisa
Masoko Mwandamizi wa DSE, Marry Kinabo, wakati akisungumza na waandishi
wa habari jana, alisema kilichochangia kushuka kwa idadi ya mauzo ya
hisa ni kutokana na wiki husika kuwa na siku pungufu za kazi na kwamba
mauzo ya hisa hizo yalifanyika kuanzia Jumatatu hadi Alhamisi ya tarehe
13 ambapo siku iliyofuata (Ijumaa) ilikuwa siku kuu ya kumbukumbu ya
Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julias Kambarage Nyerere.
Vile
vile, Kinabo alisema kuwa, kutokana na idadi ya mauzo ya hisa kushuka,
kumepelekea ukubwa wa mtaji wa soko hilo kushuka kwa 3% kutoka Trilioni
21.49 hadi Trilioni 20.8
Aidha, alitaja kampuni zinazoongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa kuwa ni CRDB kwa 53%, TCC 41% na TBL 4%.
Hata
hivyo, alisema mtaji wa makampuni ya ndani umebaki kwenye kiwango kile
kile cha Trilioni 8.13 wakati viashiria katika Sekta ya viwanda (IA),
Sekta ya huduma za kibenki na kifedha (BI) na Sekta ya huduma za
kibiashara (CS) wiki hii umebaki kama awali.