test

Alhamisi, 1 Desemba 2016

KAMANDA SIRO AFUNGUKA KUWA ZIARA ZA MAKONDA IMEMPA KIPIMO CHA UTENDAJI WAKE


KAMANDA wa Kanda Maalum ya Kipolisi ya Dar es Salaam Kamishna Simon Sirro amesema ziara ya siku kumi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi imemfanya ajue ni kiasi gani anakubaliki na kiasi gani anakubaliaka na wananchi.

Sirro amesema hayo Jumatano hii katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwa RC Makonda ya kuwashukuru watumishi wa serikali ya mkoa wa Dar es salaam pamoja na wadau mbalimbali walioshiriki katika ziara yake ya siku kumi.
“Kama Kamanda wa Kanda Maalum ya Kipolisi ya Dar es Salaam ziara imenifanya nijue wana-Dar es Salaam wanaridhika na mimi kiasi gani na hawaridhiki na mimi kwa kiasi gani nashukuru sana,” alisema Sirro.
Aliongeza,”Lakini Mh Mkuu wa Mkoa suala la pili ni kubwa sana na laaibu kwa watendaji wa Umma kutokuwa na maadili, kwenye mikutano hii ya hadhara tumeanza kukamatana sisi wenyewe. Kwa hiyo ni ombi langu kubwa sana, chombo chetu cha dola kipo kwa ajili ya ulinzi na usalama. Nilikuwa na mkuu wa mkoa kuangalia watendaji wa serikali za mtaa wapatao tisa pamoja na viongozi wa ardhi tunawashikilia kwa tuhuma za rushwa,”
Pia Kamanda Sirro amesema ameshatekeleza katizo la mkuu wa mkoa la kutowaachia askari mgambo vituo vya polisi ambapo amesema mgambo wataendelea kufanya kazi zao katika ngazi ya serikali za mtaa

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx