WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza wabunge kuuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa Dimani, Zanzibar Mheshimiwa Hafidh Ally Tahir.
Bw. Tahir amefariki saa 9 alfajiri ya kuamkia leo katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na mwili wake kuagwa katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kabla ya kusafirishwa kwenda Zanzibar kwa mazishi.
Akizungumza
katika tukio hilo, Waziri Mkuu ametoa pole kwa Spika wa Bunge,
Mheshimiwa Job Ndugai, familia ya marehemu na wabunge wote.“Tumepokea
taarifa za msiba huu kwa mshtuko mkubwa. Leo tupo katika wakati mgumu
sana. Tumeondokewa na viongozi wengi,” amesema.
Amesema
wafiwa wanatakiwa kuishi kwa upendo. “Tumuombee marehemu, tuiombee
familia iwe na moyo wa utulivu katika kipindi kigumu cha kuondokewa na
mpendwa wao.”
Bw.
Hafidh alizaliwa Oktoba 30, 1953 na aliwahi kuwa Mkuu wa Sauti ya
Tanzania Zanzibar (1970-1978) na amekuwa mbunge tangu 2005 hadi mauti
yanamkuta.Enzi ya uhai wake, alishiriki kikamilifu katika masuala ya
michezo; alikuwa mwamuzi wa soka mwenye beji ya FIFA na kocha msaidiizi
wa timu ya soka ya Bunge.
Hadi
jana, Bw. Hafidh alishiriki katika shughuli mbalimbali ikiwemo uchaguzi
wa kupata viongozi wa Tawi la Umoja wa Wabunge WanaYanga mjini Dodoma
ambapo yeye alichaguliwa kuwa Katibu.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
IJUMAA, NOVEMBA 11, 2016.