![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhRduEhyphenhyphenP8nEjQaTAflonQc-7ZBssHYHQFziFhRrURihQDLWpz_WvgKwb2ZajqFyxTc9n_4VfJ89PC2j7YyFPdzfiXAqdFnza7E-dqunfiOQ80pnyiCcfY6l2RE3p8O3ErLpziPixLnFrA/s1600/tb-joshua2.jpg)
Limekuja hili la Trump na Hilary Clinton. TB Joshua kwa Mara nyingine akaja tena na kutuambia, anamuona Mwanamke akitawala Marekani. Akabashiri ushindi kwa Hilary Clinton. Kwa mara nyingine tena Utabiri haukuwezekana! Hapa hakuna kura iliyoibiwa.
Tunaambiwa pia kuwa Mtu amepewa maono kuwa Rais Magufuli atakufa mwaka huu. Haya ni maono yake Godbless Lema na ameomba tusimshambulie yeye kwa vile ndivyo maono yake yalivyo.
Najiuliza sana. Hivi tuna Miungu wangapi? Je Mungu wa Kweli Muumba Mbingu na Ardhi anaweza kuhangaika kutuchagulia nani atutawale? Siyo kwamba Tuna miungu wanaoingilia imani zetu nasi tunawaamini na kuwakumbatia?
Kwa hili kuna haja kwa kila mwanasiasa na ikiwezekana watu wote kuhakiki imani zao. Yawezekana kuna watu wameingiliwa na shetani na wamemgeuza kuwa Mungu wao.