test

Jumatano, 9 Novemba 2016

RAIS MAGUFULI SIO WA MCHEZO KILA KUKICHA TANZANIA YAKE INAPIGA HATUA MBELE , SOMA HAPA KUJUA ZAIDI…


RAIS MAGUFULI 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania John Magufuli, ameweka mikakati imara.Hayumbishwi kwa kile anachokiiamini kuwa anafanya kwa ajili ya watanzania na sio maslahi yake.

Rais Magufuli ameweka nadhiri ya kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa kiuchumi ambayo anaitekeleza kwa kasi kubwa   
Moja ya mambo anayoyaamini kuwa yatasimamisha uchumi wa Tanzania nia pamoja na kujenga viwanda nchini. 
Katika kutekeleza agizo la Rais Magufuli tayari mfuko wa Pensheni wa PPF umeanza kutekeleza agizo hilo kwa kuingia ubia na jeshi la Magereza na kuanzisha kiwanda cha kuzalisha viatu na bidhaa za ngozi
Makubaliano haya yalisainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw.William Erio na Kamishna Jenerali wa Magereza Bw.John Minja Octoba 4, 2016 katika ukumbi wa mikutano wa makao Makuu ya Jeshi la Magereza uliopo Jijini Dar es Salaam.
katika makubaliano hayo PPF itakarabati na kuboresha miundombinu ya kiwanda cha viatu cha karanga ambacho uzalishaji ulianza mwaka 1977 na kufunguliwa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Pamoja na kiwanda cha sasa PPF itajenga kiwanda kipya cha kisasa ambacho kitakuwa kikisindika ngozi na kuzalisha bidhaa zitokanazo na ngozi kwa kutumia mashine za kisasa na teknolojia ya hali ya juu na hivyo kuongeza uzalishaji na kupanua masoko ya viatu nchini na kuongeza pato la Taifa.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx