test

Jumatano, 16 Novemba 2016

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 41 & 42


Mwandishi: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
Agnes akaingia ndani ya choo alicho elekezwa, akavua koti lake dogo alilo livaa kutokana na baridi kali, kisha akavua na gloves nyeusi alizo zivaa. Akaminya kitufe kwenye choo cha kukalia na kuyafanya maji kuweza kuzunguka, ili kumdanganya dada huyo kwamba amemaliza haja yake ya kujisaidia.

Kabla hajatoka akasikia mlango ukigongwa, jambo lililo mfanya kujiandaa na kujiweka tayari kwa lolote kisha akamruhusu mtu anaye gonga kuweza kuingia ndani. Akaingia dada mfanyakazi huku akiwa na vifaa vyake, gafla Agnes akampiga ngumi nzito shingoni dada huyo na kumfanya aanguke mzima mzima kama mzoga.

ENDELEA
Akamvuta dada huyo na kumuingiza ndani ya choo. Akatoka ndani ya choo na kuufunga mlango kwa ndani wa kuingilia ofisini hapo, kisha akasimama kwenye moja ya dirisha na kuangalia nje. Kwa bahati nzuri katika sehemu alipo simama anaweza kuona vizuri kwenye mlango wa hotel atakayo ingilia kiongozi huyo, ambapo kumejaa wananchi wengi wakiwa wamejipanga kwa kumpokea kiongozi huyo. Akachukua darubin yake, akatazama kila sehemu ya magorofa ya pembeni ili kuhakikisha usalama wake kama upo.

Alipo ridhika hakuna walenga shabaha wa serikali ambao mara nyingi hujitegega kwenye magorofa makubwa kama hayo. Akafungua kabki kake na kuanza kuchomoa kipande kimoja baada ya kingine cha silaha yake. Akaanza kuiunga kwa utaalamu mkubwa hadi ikakamilika. Akaweka magazine yenye risasi  ishirini, kisha akafunga kiwambo cha kuzuia sauti.

Akasimasa kwenye moja ya sehemu ambapo si rahisi kwa mtu wa nje kuweza kumuona. Saa yake ya mkononi akaiweka vizuri, huku ikionyesha zimesalia dakika kumi kabla ya kiongozi huyo kuweza kufika katika eneno hilo.

“Mmmmmmmm”
Agnes aliguna badaa ya kuanza kuona magari meusi yakianza kusimama katika eneo alipo ielekezea bunduki yake, kwa kutumia lensi iliyopo juu ya bunduki yake, akaona baadhi ya walinzi wa waziri huyo wakishuka kwenye magari hayo aina ya GVC. Walinzi hao wakaendelea kuwa macho huku wakijipanga mstati mmoja kuhakikisha kwamba waziri wao anakuwa salama. Kajasho kembamba kakaanza kumchuruzika Agnes, huku mapigo ya moyo yakinza kumpiga kwa mbali jambo lililo anza kumpa wasiwasi kwani katika kazi kama hiyo mtu hutakiwi kuwa na wasiwasi wa aina yoyote.

“Shitiiii!!!!”
Agnes alizungumza huku akitingisha kichwa chake, akijitahidi kutoa wasiwasi mwingi alio kuwa nao. Gari ndefu yene milango sita, ikasimama kwenye zulia jekundu la kuingialia kwenye hoteli hiyo. Walinzi wanne walio valia suti nyeusi wakaufwata mlango wa nyuma wa gari hiyo, mmoja akashika kitasa na kuufungua.

Agnes akashuhudia mguu mmoja ukitangulia kutoka kwenye gari hiyo, akatulia kidogo kutazama vizuri. Akamuona kiongozi Bwana Paul Henry Jr, akitoka kwenye gari hilo, huku akizungukwa na askari hao wanne. Mapigo ya moyo yakazidi kumuenda mbio Agnes baada ya kumuona mtoto mdogo wa kike mwenye umri wa miaka kama nane akitoka ndani ya gari hilo, na mtoto huyo anafanana sana na bwana Paul Henry Jr.
Agnes akataka kufyatua risasi ila akajihisi vibaya sana huku pumzi akiihisi inakwenda kumuishia, kila allipo jaribu kuiweka sawa bunduki yake, mikono yote ikamtetemeka, akajikuta akiwa ameduwaa akimtazama mtoo huyo aliye nyanyuliwa na bwana Paul Henry Jr na kumbeba kifuani mwake.

Bwana Paul Herny Jr akaendelea kuwasalimia wananchi walijitokeza kumpokea, huku akiwa amembeba mwanaye anaye mpenda kuliko kitu chochote na mara nyingi huwa anapenda kwenda naye kwenye dhiara kubwa kama hii ya hapa nchini Russia.
Mlio wa simu ukamstua Agnes, kwa haraka akachukua ear phone na kuiweka sikioni kisa akaminya kitufe kilichopo kwenye hiyo earphone na kuipokea simu hiyo.

“Unafanya nini wewe, muue huyo”
Sauti ya bwana Rusev alisikika kwenye simu hiyo akizungumza kwa kufoka. Agnes hakujibu kitu chochote zaidi ya kuishika bunduki yake vizuri, akayang’ata meno yake kwa nguvu na kuikaza misuli yake, ili kuuzuia wasiwasi mwingi ulio mtawala.
“Uaaaaaa”
Sauti ya bwana Rusev ikaendelea kumshawishi Agnes kufanya tukio alilo tumwa kuweza kulifanya, mshale wa msalaba uliopo kwenye lensi ya bunduki yake, ukatua kichwani bwana Paul Henry Jr, tayari kwa kufyatua risasi.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx