Mbunge
wa Ukonga kwa tiketi ya Chama cha Demokrsia na Maendeleo (CHADEMA),
Mwita Waitara anashikiliwa na Polisi katika kituo cha Polisi Chang’ombe,
Temeke, Dar es Salaam.
Mbunge
Waitara amekamatwa jana alipokuwa katika eneo la Uvikiuta alikokwenda
kufuatilia mgogoro wa ardhi wa muda mrefu kati ya wananchi wa eneo hilo
na anayedaiwa kuwa kigogo wa serikali anayetuhumiwa kuwa anataka kupora
ardhi hiyo na kuwahamisha wananchi kwa nguvu.
Mbunge
huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Kivule alifika
katika eneo hilo lenye mgogoro ambapo shughuli ya kubomoa nyumba 500 za
wananchi wa eneo hilo ilikuwa ikiendelea.
Eneo lenye mgogoro lipo mpakani mwa wilaya za Ilala na Temeke (Kivule-Ilala na Mbande-Temeke).