test

Jumanne, 25 Oktoba 2016

Chelsea yavunja rekodi ya Tottenham Hotspur kwa kocha Jose Mourinho


Licha ya kipigo ambacho Chelsea imeipa Manchester United cha nne kwa bila, jambo hilo halijaishia hapo kwani hata kwa kocha Jose Mourinho hali ni tofauti kwa rekodi alizokuwa ameziweka kuendelea kuvunjwa na timu anazokutana nazo.
Chelsea imemaliza rekodi ya Tottenham waliyokuwa wameiweka kwa Mourinho ya kuwa timu ya Ligi Kuu ya Uingereza ambayo imeifunga timu inayofundishwa na kocha huyo kwa goli nne au zaidi.
Tottehnham ilikuwa inashikiria rekodi kwa kumfunga Mourinho goli 5-3 wakati walipokutana Januari, 2015 alipokuwa akiifundisha Chelsea, na sasa Chelsea imemfunga Mourinho goli 4-0 akiwa na Manchester United.
Akizungumza kuhusu kipigo alichokipata kutoka kwa Chelsea, Mourinho alisema makosa ambayo waliyafanya dakika ya kwanza kwa kuruhusu goli ndiyo iliyosababisha timu yake kupoteza mwelekea na kukubali kichapo kutoka kwa timu yake ya zamani.
“Tulianza vibaya. Baada ya sekunde kadhaa tukafungwa goli, tukiwa tunakaribia kusawazisha, safu ya ulinzi ikafanya makosa tena na ikawa 2-0, unakuwa na mipango na hupaswi kuruhusu goli katika dakika ya kwanza. Hilo lilibadili kabisa mchezo,” alisema Mourinho.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx