Na: Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
ametoa agizo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na
Mazingira, January Makamba kuunda Kamati ya pamoja ya wataalam kutoka
Tanzania Bara na Zanzibar ili kupitia upya usajili wa meli nchini.
Makamu
wa Rais ametoa agizo hilo mbele ya Waandishi wa Habari jana Jijini Dar
es Salaam, alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya meli zilizokamatwa zikiwa
na Bendera ya Tanzania.
Mhe.
Samia amesema kuwa suala la usajili wa meli za nje ni la kawaida na
linafanywa na nchi nyingi duniani hivyo Serikali inaendelea
kushughulikia taarifa juu ya meli za nje zilizosajiliwa Tanzania zenye
tuhuma za kusafirisha silaha na dawa za kulevya kwa sababu ni kinyume
cha sheria za usajili wake.
“Kwa
kuwa uendeshaji wa biashara hii unaonekana kuleta utata na kutia dosari
kubwa kwa Taifa letu na kuharibu sifa njema kwa nchi yetu, tumeona ipo
haja ya kuunda kamati ya pamoja ya wataalam kutoka Tanzania Bara na
Zanzibar itakayoshirikisha vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya
kupitia upya usajili uliokwishafanyika na kuzihakiki taarifa za meli
zote zilizosajiliwa nchini mwetu, kuangalia mwenendo mzima wa usajili na
hatimaye kutoa mapendekezo na ushauri kwa Serikali”, alielezaa Makamu
wa Rais.
Kamati
itakaundwa pia itapitia sheria za usajili wa meli ili kuzipa nguvu
zaidi taasisi zinazosimamia usajili huo hivyo kamati itaangalia kwa
makini kodi zinazotozwa na mchango wake nchini ili zisiwe kivutio kwa
meli zisizokidhi viwango kuomba usajili Tanzania.
Aidha,
Mhe. Samia amsema agizo lakupitiwa upya sharia za usajili wa meli baada
ya kubainika kuwa wamiliki wa meli wanapenda kusajili meli zao nje ya
nchi zao kukimbia ukubwa wa kodi na sheria zinazobana pia wakala
aliyekuwa akifanya kazi hizo kwa niaba ya taasisi ya Mamlaka ya Usafiri
Baharini Zanzibar (ZMA) alishavunjiwa mkataba lakini bado anaendelea
kufanya usajili kwa kuiba bendera ya Tanzania.
Amefafanua
kuwa Sheria na Kanuni zote za usajili zinamlazimu mimiliki wa meli
kujaza fomu ya kiapo cha kutovusha biashara za dawa za kulevya wala
silaha kinyume na utaratibu hivyo Watanzania wanatakiwa kuelewa kuwa
kukamatwa kwa meli hizo sio makosa ya Tanzania ila nchi inahusishwa kwa
kuwa usajili wa meli hizo umefanyika Tanzania.
Meli
mbili, Kaluba yenye namba za usajili IMO 6828753 na Andromeda yenye
namba za usajili IMO 7614666 zilizosajiliwa Tanzania kupitia taasisi ya
Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) zilikamatwa kwa tuhuma za
kusafirisha dawa za kulevya na silaha ambapo hadi sasa tayari
zimeshachukuliwa hatua ya kufutiwa usajili.
Tanzania
ina aina mbili za usajili wa meli ambao ni usajili wa meli zenye asili
ya Tanzania na zisizo asili ya Tanzania, usajili huo ni kwa mujibu wa
mkataba wa UNCLOS wa mwaka 1982 ambapo kila nchi imepewa haki ya kufanya
usajili wa meli kwa kuzingatia mikataba ya kimataifa na sheria za nchi
husika.
SUMATRA
inaruhusu usajili wa meli zinazomilikiwa na Watanzania au kwa ubia kati
ya Mtanzania na raia wa nchi nyingine ambapo jumla ya meli 88
zimesajiliwa wakati meli za kimataifa zinasajiliwa Tanzania kupitia
Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) ambazo hadi Disemba 31, 2017
jumla ya meli 457 za nje zimesajiliwa.
0 comments:
Chapisha Maoni