Vijana wanaojiita sungusungu wakiwa na hasira kwenye mtaa wa sakina hapa mkoani Arusha imewatia nguvuni na kuwaweka chini ya ulinzi mkali wazungu 4 ambao uraia wao bao haujatambulia kwa kile kinachodaiwa kumiliki miwani yenye uwezo wa kuchungulia sehemu za siri za maumbile ya mwanadamu pindi anapovaa miwani hiyo pasipo muhusika kujijua.
Tukio hilo limetokea jana jumapili saa 5 asubuhi ambapo sungusungu hapo wakishirikiana na viongozi wa mtaa walipata taarifa kutoka kwa raia mwema dada aliyejitambulisha kwa jina la Glory *****(jina la pili kapuni)
Dada huyo Glory alieleza ya kuwa alikutana na wazungu hao akiwa anaelekea kwenye shughuli zake kisha wakamsimamisha na kuanza kumuuliza muelekeo uliopo restaurant nzuri kwa wao kuweza kukaa na kupata vinywaji ndipo alipoona wazungu hao wakiwa wanapokezana miwani hio ilionekana sio ya kawaida kama miwani iliyozoeleka, huku kila aliyekuwa akiivaa akichekana sana na kumpa mwingine ili naye aivae na kushuhudia "miundombinu mtambuka" ya dada huyo, ndipo dada aliposhtukia mchezo na kuanza kukimbia na kupiga kelele akiomba msaada ndipo watu wakaanza kukusanyika ili kujua ninikinaendelea.
Baada ya chanzo chetu kufika eneo la tukio na kuomba viongozi hao kutupa nafasi na kuongea na watuhumiwa na kuuliza kwanini bado wanaendelea kuwashikilia, sungusungu hao walikataa kata kata na kusema wakiwa tayari kuwafikisha panapohusika watatujilisha.