Gari moshi hilo la kipekee linasafiri kwa kuning'inia kwenye chuma kilicho hewani na linaweza kusafiri kwa kasi ya kilomita 60 kwa saa moja na lina ukubwa wa kubeba wasafiri 120 kwa kila bogi.
Kwa sasa linaendelea kufanyiwa majaribio kabla ianze kusafirisha watu kikamilifu
Mashirika ya habari yalisema Treni hiyo itapunguza pakubwa gharama za usafiri kwani inatumia betri ikilinganishwa na Treni zingine ambazo hutumia nguvu za umeme au mafuta ya diesel
Mkuu wa ubunifu wa mradi huo Bw Zhai Wanming alinukuliwa akisema "Majaribio yatafanywa kwa makundi ya maelfu ya kilomita kuhakikisha kiwango cha ubora wake kabla ianze kuhudumu rasmi"
Mradi kama huo unatarajiwa kuanzishwa pia katika mji wa Shanghai nchini humo mwaka ujao.