test

Jumamosi, 10 Septemba 2016

Visa mkasa: Wabunge nao Waonja Utapeli kwa njia ya simu



USIKURUPUKE unapopokea ujumbe wa simu ya mkononi ukikuomba utume fedha kwa mtu yeyote. Hata kama utaona ujumbe huo umetumwa kwa namba ya mtu wa karibu yako sana, zingatia ushauri wangu, tafakari kwanza na jiridhishe kabla ya kutuma.
Kama ni ujumbe wa kuombwa fedha na mtu unayedhani unamfahamu (kupitia namba yake), kabla ya kutuma, jiridhishe kwanza kwa kumpigia simu. Ukiona simu haipokewi, achana nayo hadi yeye atakapokupigia na kujiridhisha ndiye aliyetuma ujumbe.

Aidha, unapopokea ujumbe wa maneno au hata kupigiwa simu na mtu (hasa usiyemjua) ukikutaka uingie kwenye ‘dili’ lolote la kifedha, tuliza moyo. Acha tamaa. Jicho langu limelazimika kuangazia suala hili kutokana na ukweli kwamba, wapo watu wameibiwa fedha kwa namna tofauti kupitia mawasiliano ya simu.
Vipo visa vingi vya namna hii. Wapo ambao yakishawakuta hawasemi, bali wanabaki kuugulia maumivu kimyakimya.
Baadhi ya wabunge walieleza namna walivyojikuta wakituma fedha nyingi wakidhani wanazituma kwa ndugu, kumbe ni kwa matapeli.
Waheshimiwa hawa waliibiwa kwa mbinu ambayo wezi hawa wamekuwa wakiingilia mtandao wa mtu kwa dakika kadhaa na kutumia namba ya simu ya mtu aliyezimiwa, kutapeli watu wengine. Mbunge mmoja alishuhudia alivyotuma Sh 800,000 baada ya kupokea ujumbe kutoka namba ya simu ya ndugu yake.
Kumbe hakuwa nduguye, bali matapeli waliingilia mtandao wake. Mwingine akaeleza mfanyakazi wake alivyotuma Sh milioni 1.6 baada ya kupokea meseji iliyoonesha ni simu ya bosi wake ikimtaka amtumie kiasi hicho cha fedha.
Ipo mifano mingi ya wizi na utapeli unaofanyika kwenye simu za mkononi. Na kila siku, hawa wezi wa kimtandao wamekuwa wakibuni mbinu mbalimbali.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx