test

Jumapili, 13 Septemba 2015

Wema: Ningeenda Ukawa, kaburi la baba yangu lingetitia




 Staa wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
Ohoo! Habari ikufikie kwamba, staa wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amefunguka kuwa kama angetoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuhamia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), siku hiyo kaburi la baba yake, marehemu Isaac Abraham Sepetu lingetitia.

Akizungumza na gazeti namba moja la mastaa Bongo, Ijumaa Wikienda, Wema alitiririka kwamba kama angetoka CCM na kwenda Ukawa angekuwa amefanya kosa kubwa katika maisha yake na kumchukiza marehemu baba yake.
“Siku ambayo ningehama tu hata kaburi la baba yangu lingetitia kwani alikuwa ni mwanachama mtiifu wa chama tawala na kamwe asingependezwa na kuhama kwangu kwenda upinzani, kwa kweli naapa sitaondoka CCM ng’o,” alisema Wema.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni