Aliyekuwa
Waziri Mkuu wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward
Lowassa, leo amewasili Bukoba mkoani Kagera kuwatembelea na kuwajulia
hali waathirika wa tetemeko la ardhi.
Tetemeko la ardhi lililotokea Bukoba mkoani Kagera Septemba 10 lilisababisha vifo vya watu 19 huku wengine zaidi ya 250 wakiachwa na maejeraha mbalimbali.
Alipofikika
katika uwanja wa ndege wa Bukoba, Edward Lowassa aliyeambatana na
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema , Sheikh Katimba, Khamis Mgeja na
Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare waliongozana hadi eneo la
Hamugembe na Kashai kujionea madhara ya tetemeko la ardhi.
Akizungumza
kwa nyakati tofauti na wananchi wa maeneo hayo, Lowassa aliwapa pole
sana kwa yote yaliowafika na kusisitiza kwamba anaamini serikali
itachukua jukumu la kuwasaidia.
Aidha,
amesema kuwa msaada wake yeye atampatia Mkuu wa Mkoa, Meja Jenerali
Mstaafu, Salum Kijuu ili uweze kuwasaidia wananchi wa Kagera.