Gazeti la Jambo leo lmeripoti kuwa watu wanaokula nyama choma kwenye baa wako hatarini kuathirika kiafya kutokana na ukiukwaji wa utaratiu kuanzia zinapoandaliwa hadi anapopelekewa mlaji.
Jambo Leo imeeleza kuwa uchunguzi uliofanywa na mamlaka ya chakula na dawa Tanzania ‘TFDA’ umebaini kuwa wanokula nyama hasa baa wako haratarini kuathirika kiafya kwa namna mbalimbali kwa sababu hiyo TFDA imependekeza kuwa wanaoandaa nyama hiyo wanapaswa kuabadili tabia kwa kuhakikisha imekaguliwa na mabwana afya, inachomwa kwa uangalifu na anapelekewa mteja ikiwa bao ya moto.
Gazeti hilo limeeleza kuwa kwa kuwa nyama ni sehemu ya vyakula ambayo inaonekana kuvuta hamu ya kula kwa watu wengi, wanywaji baa hupendelea kunywa nyama zaidi kama moja ya kiamasidhio cha starehe ya kupata kilevi, nyama inayotumiwa zaidi ni ile inayotokana na ng’ombe, nguruwe, mbuzi, kuku na kondoo hata hivyo inaweza kuchafuliwa na vimelea mbalimbali vya maradhi endapo kanuni bora za usafi hazitazingatiwa wakati wa uaandaji na utunzaji wa nyama hiyo.
TFDA inaeleza kabla ya kuliwa nyama huweza kuandaliwa kwa njia ya kuchomwa kwenye jiko la mkaa kuni, jiko la umeme au gesi hadi hapo itakapobadiliaka rangi kuashiria kuwa imeiva.Utarishaji wa aina hii hupendwa na walaji wengi kwa kuwa unaaminika, hii ni baada ya kupika kwa kutumia maji au mafuta yake hivyo kuwa na radha nzuri.
Utayarishaji wa nyama kwa njia ya kuchoma hufanyika kwa wingi kwenye maeneo ya baa, hotel, migahawa na hata majumbani, hata hivyo baadhi ya tafiti zinaonyesha mara nyingi nyama inayochomwa haivi vizuri na hivyo kubaki na vimelea vya maradhi ambavyo ni hatari kwa afya ya mlaji, hali hii inaweza kuwa mbaya zaidi hasa nyama inayochomwa inapokuwa haikukaguliwa na kupitishwaa na mamlaka husika kuwa inafaa kwa matumizi ya binadamu.
Source: Jambo Leo