test

Alhamisi, 15 Septemba 2016

Kanitafutia Kazi Sasa Nimekua Mtumwa wa Ngono Kwake


Hi guys, niaje?

Ni miezi miwili sasa tangu nimeacha kazi kampuni ya zamani, na sasa nipo kwenye kampuni nyingine, hii kazi mpya nimetafutiwa na Boss wangu ambae ndie mkuu wa idara yetu, nimepanda cheo kidogo, kule nilikuwa Karani na huku kupya mimi ni Supervisor.


Sasa huyu Boss alieniingiza kazini nimekua na urafiki nae tangu nimeingia hapa, kitu kinachonikwaza ni mwenendo wa huyu Boss wangu, yaani nimekua kama mtumwa, wakati wote anataka tufanye ngono, jioni wakati wa kuondoka anataka tubaki ofisini kwake, najikuta nafika home saa tatu hivyo kumkuta Mr wangu amesharudi Muda, inakua ugomvi, inabidi nimdanganye kuwa kazi mpya imekua too demanding kwangu, nachelewa kutoka.

Weekend ni hivyo hivyo, inabidi nisingizie home kuwa tunatakiwa kazini hata Jumapili, nimejikuta naishi kama mtumwa kwa sababu ya hii kazi aliyonipa huyu Boss, maneno maneno yamekua mengi hapa kazini miongoni mwa Staff wenzangu kuhusu mwenendo wangu na huyu Boss, nina wasi wasi maneno haya yanaweza kumfikia Mr wangu ikawa shida.

Natamani kuirudia ile kazi yangu ya awali, kazi hii mpya napata mshahara mzuri lakini nimekua kama mtumwa, wakati mwingine nikionesha dalili za kumgomea kubaki jioni anakua mkali na kuanza vitisho kwamba eti '' unasahau nani kakuweka hapo ''Inabidi tu nishiriki nae ingawa sipendi.

Naombeni ushauri nifanyeje?

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx