Polisi jijini Dar es Salaam wamewakamata watu 33 wakiwamo vijana wanaopenda kukaa ufukweni maarufu ‘beach boys’ kwa tuhuma za kuwahadaa wasichana kimapenzi.
Vijana hao, wanadaiwa kuwarubuni wasichana kuwa watawafundisha kuogelea lakini baadaye huwalazimisha kufanya ngono wakiwa majini.
Vijana hao, wanadaiwa kuwarubuni wasichana kuwa watawafundisha kuogelea lakini baadaye huwalazimisha kufanya ngono wakiwa majini.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema watuhumiwa hao wamekamatwa baada ya askari kufanya msako na kukutwa wakifanya mapenzi kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi.