test

Jumatano, 28 Septemba 2016

Diamond Platinumz kumpa shavu lingine Saida Kalori


Baada ya Diamond Platnumz kurudia ngoma ya “Salome” ya Saida Kalori, Hili ni shavu jingine tena laDiamond kwa Saida Kalori.
Najua ngoma ya Diamond ya “Salome” ni kali zaidi na imesababisha Tanzania kumkumbuka tena Legendary Saida Kalori kwani kwa wakati ukizisikia Maria Salome na Salome ya Diamond zikipigwa kwa pamoja au moja moja ni kawaida kwani hii ni win win Situation kwa wasanii wote wawili, Sasa Diamond amefunguka kwamba kuna shavu jingine jipya linakuja kati yake yeye na Legendary Saida Kalori.

Akiongea na Perfect255, Diamond Platnumz amesema kwamba anafikiria siku ambayo atakuja kuperforme Dar jukwaani basi lazima atamuhusisha na Legendary Saida Kalori na kingine Kikubwa Diamond platnumz amesema kwamba inawezekana pia yeye na Saida Kalori kufanya kolabo ya pamoja.

“Tulizungumza hilo pia na ninafikiri siku ya kwanza nitakayo performe nyimbo Dar es salaam inawezekana nikamleta Saida tukaperforme pamoja” Alisema Diamond

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx