Mama Diamond, Bi Sandra, amemtonesha mchumba wa mwanae, Zari pale panapomuuma zaidi.
Amempongeza
ex wa Diamond, Wema Sepetu katika birthday yake, Jumatano hii, Septemba
28, siku chache tu baada ya kumkaushia Zari kwenye birthday yake –
ajabu!
"Happy
birthday.. Mamy akee @wemasepetu mungu akuongezee umri na akujali kheri
akufungulie Mlango wa baraka kwa kila uliombalo.Aminππ πππ,” ameandika Bi. Kendrah Jumatano hii.
Post
hiyo inadhihirisha uvumi wa muda mrefu kuwa Zari haelewani na mama mkwe
wake huyo pamoja na ndugeze wengine wake Diamond. Wifi yake, Esma naye
alimkaushia raia huyo wa Uganda mwenye makazi yake Afrika Kusini.
Kwa muda sasa Zari na mama mkwe wake hawana maelewano mazuri
Minong’ono
inadai kuwa Zari hakubaliki ukweni kutokana na kupenda maisha ya
kizungu, kutawala mipango ya Diamond na huenda ndio chanzo cha Bi Sandra
kuondoka Madale, nyumbani kwa staa huyo.
Pamoja
na Zari kutokubalika ukweli, Diamond haoneshi kushtushwa na hali hiyo
kwakuwa hivi karibuni alimzawadia nyumba yenye thamani ya shilingi
milioni 396 ya Afrika Kusini pamoja na kumpeleka visiwani Zanzibar
kusherehekea birthday yake.
Labda
ndugu za Diamond inabidi waukubali tu ukweli mchungu kuwa Zari sasa
ndio kila kitu kwa staa huyo. Wakiwa na mtoto mmoja sasa, Tiffah, wawili
hao wanatarajia kuongeza mtoto wa pili December mwaka huu.