Pia, mahakama hiyo imemtaka mshtakiwa huyo kumlipa mkewe Sh5 milioni ambazo ni thamani ya dhahabu aliyoiba.
Akisoma
hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Said Mkasiwa alisema
ameridhishwa na mashahidi watatu wa upande wa mashtaka waliotoa dhidi ya
mshtakiwa huyo.
Alisema upande wa Jamhuri uliwasilisha mashahidi watatu ambao wamethibitisha shtaka hilo pasi na kuacha shaka.
“Kutokana
na ushahidi uliotolewa mahakamani hapa nimejiridhisha pasi na kuacha
shaka hivyo mshtakiwa ninamtia hatiani kama alivyoshtakiwa,’’ alisema Hakimu Mkasiwa na kuongeza:
“Hivyo Mahakama imekuhukumu kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kupatikana na kosa la kuiba seti moja ya dhahabu yenye ya Sh5 milioni.”
“Hivyo Mahakama imekuhukumu kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kupatikana na kosa la kuiba seti moja ya dhahabu yenye ya Sh5 milioni.”
Kabla
ya kutolewa kwa adhabu hiyo, Wakili wa Serikali, Sylvia Mitanto
aliiomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwa
watu wengine wenye tabia kama hizo.
Akijitetea
kwa nini asihukumiwe kifungo hicho, Janga aliiomba Mahakama impunguzie
adhabu kwa madai kuwa hali yake ya kiafya siyo mzuri. Aliomba apewe
kifungo cha nje.
Kwa
mujibu wa hati ya mashtaka, Janga alitenda kosa hilo Oktoba 27, 2014
katika maeneo ya Upanga wilayani Ilala. Alidaiwa kuiba dhahabu ambayo ni
cheni ya shingoni, cheni ya mkononi na hereni mali ya mkewe.
Inadaiwa kuwa wawili hao walidumu katika ndoa kwa mwezi mmoja.