Msanii wa Kenya mwenye makazi yake nchini Qatar, Sheikha ameonesha jeuri ya pesa na kutangaza vita kwa madiva wote wanaodaiwa kuwa matajiri akiwemo Akothee na Vera Sidika.
Sheikha ambaye hivi karibuni aliachia wimbo wake mpya uitwao Yebede, amesema anataka kumuonesha Akothee na wengine nini maana ya kuwa na fedha.
Anadai kuwa wanawake wengi wa Kenya wamekuwa wakionesha jeuri ya pesa ambazo sio zao bali za mabwana zao wazee wanaojulikana kama sponsors.
Sheikha amewahi kumkosoa Akothee kwa kujiita ‘bosylady’ aliyejipatia umaarufu Kenya kwa matumizi yake na utajiri mkubwa na kudai kuwa bado hajafikia level hiyo.
Hivi karibuni Akothee alitangaza mchongo kwa wasichana kutuma video wakicheza nyimbo zake na mshindi kupewa shilingi 10,000 za Kenya. Sheikha naye ametangaza dili kama hilo kwaajili ya ngoma yake Yebede ambapo naye mshindi atapewa KSh 10,000.
Je vita kati ya Akothee na Sheikha ndiyo imeanza? Akothee hadi sasa ana collabo kubwa mbili na Diamond na Flavour.