Mazoezi kwa wanajeshi ni kitu cha muhimu sana. Majeshi duniani huhakikisha kuwa wanawafunza wanajeshi wao mafunzo ya kuikakamavu kuweza kuwajenga kimwili na kiakili ili kuweza kupambana na hali tofauti tofauti wanazokumbana nazo wakiwa vitani au katika mazingira mengine.
Hizi hapa ni picha za majeshi tofauti tofauti duniani zikionyesha mazoezi magumu ambayo huwa wanfanya.
Wanajeshi wa China wakifanya mazoezi kwenye matope.
Mwanajeshi wa China akitambaa chini ya nyaya zinazowa waka moto wakati wa mazoezi.Baada ya kutambaa na kufanya mazoezi kwenye moto, sasa wanafanya mazoezi ya viungo.Mazoezi wakati mwingine huwa ni adhabu kwa wanajeshi. Hapa wanajeshi wa China wakitakiwa kubana pumzi na kuweka uso ndani ya maji.Wanajeshi wa China wakifanya mazoezi yao kwenye barafu. Maeneo haya yana baridi ya hali ya juu.Wanajeshi wa kitengo maalum cha kivita nchini Korea ya Kusini wakifanya mazoezi yao kwenye barafu.Mwanajeshi wa nchini Canada akifanya mazoezi katika maji yenye barafu ikiwa ni mazoezi ya NATO.Wanajeshi wa majini wa Marekani pamoja na Korea Kusini wakifanya mazoezi pamoja katika milima nchini Korea Kusini.Wanajeshi wa Marekani wakiwa mazoezi Thailand. Katika kujifunza namna ya kushi katika hali ngumu, wanajeshi hao hulazimika kunywa damu ya Chatu.Mwanajeshi wa Marekani wakiwa mazoezini ambapo anaruka kutoka kwenye helikopta akiwa na mbwa anayemfanyia mazoezi.Wanajeshi nchini Japan wakifanya mazoezi ya kuning’ia kwenye helikopta kwa kutumia kamba.Ili mwanajeshi ahitimishe mafunzo ya wiki tisa nchini Taiwan, unatakiwa kutembea umbali wa futi 150 juu ya mawe na miamba.Belarus, ili uweze kuwa mmoja wa kundi la Red Berets, unatakiwa kupita kwenye vikwanza mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupita juu ya boma kwa kutembea.Mmoja wa wanakundi wa Red Berets akiwa amefukiza kichwa chake ndani ya matofali yenye moto ikiwa ni sehemu ya maonyesho ya kundi hilo kila mwaka.Mazoezi ya uvumilivu ni muhimu sana, wanajeshi wa Israel kila mmoja analazimika kutembea umbali wa maili 43 (69 km) ikiwa ni sehemu ya mazoezi.Wanajeshi wa Palestina wakifanya mazoezi ya kuruka angani.Kundi la Kurdish YPG nchini Syria likifanya mazoezi katika viunzi vyenye motoWanajeshi wa Kishia nchini Iraq wakifanya maonyesho ya mazoezi yao wakati wa mahafali yao.Wanajeshi wengine wa Kishia nchini Iraq ili kuweza kuhitimu mafunzo yao wanalazimika kutambaa kwenye mchanga/udongo jangwani