Benki
ya NMB imeendelea kutanua mtandao wa matawi yake nchini ili kuwa karibu
zaidi na wateja wake. Mwishoni mwa wiki iliyopita, NMB ilizindua tawi
jipya la NMB Rock City lililopo ndani ya jengo jipya la kibiashara la
Rock City jijini Mwanza.
Tawi
hili linafanya jumla ya matawi ya NMB kwa Mwanza mjini kufikia matano
na 28 kwa kanda nzima ya ziwa ni imani ya NMB zinduzi huu unaleta
tumaini jipya kwa wateja wa NMB jijini Mwanza na kanda ya ziwa kwa
ujumla.
Huduma zinazotolewa na tawi hili jipya ni pamoja na kufungua akaunti, mikopo, huduma ya fedha za kigeni, huduma za kuweka na kutoa fedha.
Huduma zinazotolewa na tawi hili jipya ni pamoja na kufungua akaunti, mikopo, huduma ya fedha za kigeni, huduma za kuweka na kutoa fedha.
Katika
kuhakikisha kuwa NMB inahudumia makundi mbalimbali ya wateja wake
kulingana na mahitaji yao ya kifedha, wiki iliyopita, benki iliendesha
mkutano wa Klabu ya Biashara uliowakutanisha pamoja zaidi ya wateja 300
wanaohudumiwa na matawi ya NMB ya jijini Mwanza.
Baadhi ya faida zilizopatikana katika mkutano huo ni pamoja na mafunzo ya jinsi ya kukuza biashara, elimu ya mlipa kodi, jinsi ya kutunza daftari la biashara na njia mbalimbali za kuboresha biashara.
Baadhi ya faida zilizopatikana katika mkutano huo ni pamoja na mafunzo ya jinsi ya kukuza biashara, elimu ya mlipa kodi, jinsi ya kutunza daftari la biashara na njia mbalimbali za kuboresha biashara.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza John Mongela (katikati) akikata utepe kuzindua tawi
la Rock City Mall la benki ya NMB jijini Mwanza, wa tatu kushoto ni
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa NMB Bi Magreth Ikongo na wa tano
kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa NMB Ineke Bussemaker.
Meneja
wa NMB kanda ya ziwa- Abraham Augustino akiongea katika mkutano wa
klabu ya biashara uliofanyika jijini Mwanza wiki iliyopita. Zaidi ya
wateja 300 walihudhuria mkutano huo ambapo pamija na mambo mengine
walipata mafunzo ya jinisi ya kukuza biashara, elimu ya mlipa kodi na
njia mbalimbali za kuboresha biashara.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurungezi ya NMB- Margaret Ikongo akizungumza katika mkutano wa Klabu ya Biashara jijini Mwanza.