test

Jumamosi, 27 Agosti 2016

Genk ya Mbwana Samatta YAPANGWA KUNDI F EUROPA


Genk anayoichezea Mbwana Samatta imepangwa kundi F michuano ya Europa pamoja na Athletic Bilbao, Rapid Vienna na Sassuolo
Robin van Persie atakabiliana na Manchester United katika michuano ya Europa baada ya Fenerbahce kupangwa kundi moja na timu ya zamani ya Mdachi huyo.
United hawatapata tabu kupita katika kundi hilo ambalo pia Feyenoord na timu isiyo maarufu sana Zorya Luhansk.
Southampton ni timu pekee ya Uingereza iliyobakia kwenye michuano baada ya West Ham kutolewa, itacheza dhidi ya Inter Milan, Sparta Prague na Hapoel Beer Sheva.
Dundalk ya Ligi ya Ireland imepangwa kucheza dhidi ya Zenit St Petersburg, AZ Alkmaar na Maccabi Tel-Aviv.
Bosi wa United Jose Mourinho amekiri kuwa haijui sana timu ya Ukraine Zorya lakini amefurahia kupangwa kuzikabili Fenerbahce naFeyenoord.
"Tunajua kwamba ushindani wa michuano hii si kama ule wa Ligi ya Mabingwa lakini Manchester United itacheza dhidi ya klabu zenye utamaduni kama Fenerbahce na Feyenoord jambo ambalo ni jema kwetu."
"Tunajua kwamba kundi hili litakuwa gumu, lakini ni jambo jema. Ni jema kwa mashabiki na kwa wachezaji kwa sababu litaleta hamasa."
Droo kamili Europa hii:
Kundi A: Man Utd, Fenerbahce, Feyenoord, Zorya Luhansk
Kundi  B: Olympiacos, Apoel Nicosia, Young Boys, Astana
Kundi  C: Anderlecht, St Etienne, Mainz, Qabala
Kundi  D: Zenit St Petersburg, AZ Alkmaar, Maccabi Tel-Aviv, Dundalk
Kundi  E: Plzen, Roma, Austria Vienna, FC Astra Giurgiu
Kundi  F: Athletic Bilbao, Genk, Rapid Vienna, Sassuolo
Kundi  G: Ajax, Standard Liege, Celta Vigo, Panathinaikos
Kundi  H: Shakhtar Donetsk, Braga, Gent, Konyaspor
Kundi  I: Schalke 04, FC Red Bull Salzburg, Krasnodar, Nice
Kundi  J: Fiorentina, PAOK Salonika, Liberec, Qarabag
Kundi  K: Inter Milan, Sparta Prague, Southampton, Hapoel Beer Sheva
Kundi  L: Villarreal, Steaua Bucharest, FC Zurich, Osmanlispor

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx