Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba amezungumza na kusema kuwa CHADEMA wasithubutu kuandamana kwani kwa kufanya hivyo si kuwa watakuwa wanatingisha kiberiti cha njiti, bali watakuwa wanachezea gesi. Amesema kuwa sio kila kitu mtu anatakiwa kujaribu kwa sababu vingine huenda vikakuumiza.
Waziri
ameyasema maneno hayo akiwaasa viongozi wa CHADEMA kutupilia mbali
mpango wa maandamano na mikutano ya siasa nchi nzima Septemba Mosi.
Kufuatia kauli hiyo ya Waziri, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema haya. Msikilize hapa chini.