Kwamba
tarehe 21.08.2016 majira ya 10:00 usiku katika eneo la club ya villa
park resort kata ya kirumba wilaya ya ilemela mkoa wa mwanza, askari
namba g.5092 pc john nyange wa ofisi ya mkuu wa upelelezi na makosa ya
jinai mkoa wa mwanza (rco), aliuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha
kali eneo la shingoni na mtu aliyekuwa anaugomvi nae.
Inadaiwa
kuwa marehemu alikua na ugomvi wa muda mrefu na mtu aliyejulikana kwa
jina magina hussein miaka [27] fundi computer msukuma na mkazi wa mtaa
wa kigoto, ambapo marehemu alikuwa akimdai bwana magina hussein computer
aina ya laptop. Ndipo usiku wa leo majira tajwa hapo juu walikutana
eneo la club ya villa park huku mtuhumiwa wa mauaji hayo ikisemekana
kuwa alikuwa na wenzake watano ndipo walimvamia na kumchoma na kitu
chenye ncha kali shingoni na kufariki dunia njiani wakati akipelekwa
hospitali.
Marehemu
kwa sasa alikuwa ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha stefano moshi memorial
university college cha mjini moshi, alikuwa anasomea shahada ya sayansi
ya habari na mawasiliano mwaka wa pili, aidha alirejea mwanza baada ya
kupata likizo kuja kuiangalia familia yake ndipo umauti ukamkuta.
Watuhumiwa
sita akiwepo magina selemani ambaye alikuwa na ugomvi na marehemu
pamoja na wenzake watano wamekamatwa, wapo katika mahojiano na jeshi la
polisi huku uchunguzi kuhusiana na kifo hicho ukiwa bado unaendelea,
pindi uchunguzi ukikamilika watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani,
mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya rufaa ya bugando kwa
uchunguzi.
Kamanda
wa polisi mkoa wa mwanza naibu kamishina wa polisi ahmed msangi anatoa
wito kwa wananchi wa jiji na mkoa wa mwanza, kwamba jeshi la polisi mkoa
wa mwanza limesikitishwa na kifo cha askari huyu kwani limempoteza
askari kijana ambaye bado jeshi lilikuwa linamtegemea.
Lakini
pia anawataka watu wenye tabia za kujichukulia sheria mkononi kwa
kuwapiga wengine hadi kufikia kupoteza maisha kuwa wanafanya kosa la
jinai, na kama watu wanadaiana wafuate taratibu za kisheria zilizowekwa
ili kuepusha vifo vinavyoweza kuepukika, hivyo jeshi la polisi
linawataka kuacha tabia hiyo mara moja kwani hatua kali za kisheria
zitachukuliwa dhidi yao.
Imetolewa na:
Dcp: ahmed msangi
Kamanda wapolisi (m) mwanza