Wafanyabiashara
nchini wanauwezo wa kupata mikopo ya hadi dola milioni 500 za Marekani
katika benki ya Maendeleo ya Biashara Afrika –AFREXIMBANK
benki ya Maendeleo ya Biashara Afrika –AFREXIMBANK
Wafanyabiashara nchini wanauwezo wa kupata mikopo ya hadi
dola milioni 500 za Marekani katika benki ya Maendeleo ya Biashara
Afrika –AFREXIMBANK- kwa sababu Tanzania ni miongoni mwa wamiliki wa
benki
hiyo.
Akizungumza na wafanyabiashara wa Tanzania jijini DSM, Mkurugenzi wa maendeleo ya miradi wa benki hiyo JOHN KOFI amesema mikopo hiyo ni ya muda mfupi na ni kwa ajili ya wafanyabiashara waliowekeza kwenye sekta za viwanda, biashara, madini na hoteli.
Naye naibu gavana wa benki kuu LILA MKILA amesema serikali imewekeza fedha nyingi kwenye benki hiyo ili kuruhusu wafanyabiashara, zikiwemo taasisi za fedha kupata mitaji kwa urahisi.
Wakati huo huo idadi ya hoteli za kitalii zinazomilikiwa kwa asilimia mia moja na watanzania inaongezeka baada ya mitaji kuanza kupatikana kwa urahisi.
Meneja masoko wa hoteli ya kitalii ya Mbezi Garden ya jijini DSM RICHARD MOSHA amesema hoteli nyingi za kitalii nchini zimejengwa na watanzania kutokana na upatikanaji kwa urahisi wa mitaji.

0 comments:
Chapisha Maoni