MGOMBEA mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu ameanza ziara yake mkoani Ruvuma akiinadi ilani ya chama hicho huku akiahidi neema kwa wakulima wa kahawa na mahindi wa mkoa huo.
Bi.
Samia Suluhu ambaye amehutubia mikutano mitatu katika majimbo mawili ya
mkoa wa Ruvuma yaani Jimbo la Nyasa na Mbiga Vijijini, akizungumza
katika mikutano yake amesema serikali itakayoundwa na CCM endapo
itashinda itahakikisha inashusha umeme katika vijiji vyote vya mkoa huo
kwa awamu ili kuchochea maendeleo ya wananchi.
Alisema
kwa kuwa mkoa huo unazalisha mazao ya mahindi na kahawa serikali
itahakikisha inaanzisha viwanda eneo hilo vya kusaga na kuandaa unga wa
mahindi kwa wakulima na kuwawezesha ili wauze unga na kunufaika zaidi
tofauti na ilivyo kwa sasa ambapo wamekuwa wakilanguliwa.
Alisema
viwanda vingine ambavyo Serikali ya CCM itavianzisha ni pamoja na
viwanda vya kubangua kahawa na kuiandaa kikamilifu tayari kwa kutumika,
jambo ambalo alisema licha ya kuongeza thamani ya zao hilo itaongeza
ajira kwa vijana na kuchochea uchumi wa wakulima eneo hilo.
Akizungumzia
miundombinu ya barabara ambayo bado ni changamoto kwa mkoa huo hasa
vijijini alisema serikali itakayoundwa na CCM chini ya uongozi wa Dk.
John Pombe Magufuli pamoja na yeye watahakikisha wanajenga na kuboresha
barabara za maeneo hayo ili ziweze kupitika kwa uhakika.
Hata
hivyo kiongozi huyo amesema Serikali itakayoundwa na CCM endapo
itashinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2015 imejipanga kuboresha vizuri
huduma za afya kuondoa ukiritimba na rushwa, elimu kwa kutoa elimu bure
toka darasa la kwanza hadi kidato cha nne pamoja na ujenzi wa mabweni na
uwezeshaji vijana na akinamama kiuchumi popote walipo mjini na
vijijini.
Ziara
ya mikutano ya kampeni ya mgombea mwenza huyo wa urais tiketi ya CCM,
inaendelea leo katika Mkoa wa Ruvuma na ataingia Jimbo la Tunduru
kuendelea kuinadi ilaya ya chama hicho kuomba ridhaa kwa wananchi ili
waweze kurejeshwa madarakani na kuunda dola.
0 comments:
Chapisha Maoni